TUCTA YATOA TAARIFA RASMI YA MAADHIMISHO YA SHEREHE MEI MOSI KITAIFA MWAKA 2024

 




MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA ME MOSI KITAIFA 2024

RAIS wa shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini  Peter Nyamhokya ametangaza Taarifa Rasmi ya maadhimisho ya Sherehe ya Mei mosi kitaifa mwaka huu 2024,Taarifa hiyo ametoa Leo Jumatano April 17,2024 Jijini Arusha 

Akizungumza na waandishi wa Habari Rais Tumaini Peter Nyamhokya amesema" Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa Afya njema na kutufikisha salama siku ya leo. Kipekee kabisa napenda kuwashukuru sana nyinyi waandishi wa Habari kwa kuitikia wito wetu,natambua mna majukumu mengi lakini mmetuheshimu sisi Wafanyakazi na kukubali kuja kutusikiliza ili mkauhabarishe umma jambo hili muhimu. Kwaniaba ya Wafanyakazi nasema Asanteni sana"



"Lengo la kukutana nanyi siku ya leo ni kutoa taarifa rasmi kwa Vyombo vya Habari kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa kwa Mwaka huu 2024. Kwa niaba ya Wafanyakazi wote nchini napenda kuwajulisha rasmi kwamba Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa kwa Mwaka 2024 yatafanyika Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Mgeni Rasmi atakuwa ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."alisema Rais Nyamhokya

Kwa upande Rais Tumaini Nyamhokya alisema"Kama Wafanyakazi kwa pamoja kupitia kikao cha Kikatiba cha Baraza Kuu TUCTA chenye mamlaka ya kuridhia Kaulimbiu kilichofanyika tarehe 21Machi 2024, Mkoani Morogoro tulikubaliana Kaulimbiu ya Mei Mosi kwa Mwaka 2024 ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”. Kaulimbiu hii inaendana na uhalisia wa Maisha ya Mfanyakazi kwa sasa kwani gharama za Maisha zimepanda na mishahara haikidhi mahitaji ya kila siku ya mfanyakazi. Pia mishahara ikiwa Bora itawezesha mafao kuwa bora pia wakati wa kustaafu."

Aidha Rais Nyamhokya amefafanua Umuhimu wa Mei Mosi amesema"Hivyo basi tumeona ni vyema kutumia Siku yetu hii muhimu ya Sherehe za wafanyakazi kuikumbusha Serikali na waajiri wote umuhimu wa kuwa na Mishahara bora inayoendana na hali halisi ya maisha tukiwa kazini na baada ya kustaafu.


Pia Rais Tumaini ameeleza waratibu wa maadhimisho ya Sherehe ya Mei mosi amesema"Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu 2024 yameratibiwa na Vyama vyote 13 vinavyounda Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)ambavyo ni; - CHODAWU, COTWU (T), CWT, DOWUTA, RAAWU,TALGWU, TAMICO, TASU, TEWUTA, TRAWU, TPAWU, TUGHE naTUICO. Aidha, TUCTA imeshirikiana na vyama vyote vilivyo nje ya TUCTA vilivyojitokeza katika maandalizi haya." 


Pia ameongeza Kuwa Maadhimisho haya yataenda sambamba na Michezo mbalimbali ya Meimosi itakayofunguliwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 20 Aprili 2024 na Wazri wa Kazi, Vijana Ajira na Watuwenye Ulemavu Mh. Deogratious Ndejembi.


Mwisho Rais wa TUCTA Tumaini Peter Nyamhokya ametoa Rai kwa niaba ya Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi"TUCTA inatoa rai kwa Wafanyakazi wote waliopo Mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani kujumika kwa pamoja siku ya kilele cha maadhimisho ya Mei mosi Kitaifa ili tusherekee kwa pamoja na kuienzi siku hii muhimu kwa wafanyakazi Duniani."







Post a Comment

0 Comments