VISION 2030 KUGUSA MAISHA YA KILA MTANZANIA WA KAWAIDA – MAHIMBALI

 



Na  MWANDISHI WETU


Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amesema kuwa dhumuni au dhana kubwa ya 'Vision 2030' ni kuhakikisha kila Mtanzania wa kawaida anajua ni kwa namna gani Sekta ya Madini inamgusa kwenye maisha yake.
 
Amesema hayo leo Novemba 06, 2023, jijini Dodoma, wakati akizungumza katika kipindi cha runinga na radio cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi Media. 

“Vision 2030 inalenga kuleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Madini kwa kuboresha maisha ya Watanzania wa kawaida, uchumi kwa ujumla sambamba na kufungamanisha sekta zingine tunataka wananchi wanufaike na uwepo wa rasilimali hii.” amesema Mahimbali. 

Amesema kuwa kupitia utafiti wa kina wa jiosayansi kutakuwa na kanzidata ya kutosha kuhusu miamba yote yenye madini, maji pamoja na aina ya udongo kwa sehemu husika, hapo tayari sekta ya madini imefungamanisha sekta ya kilimo na maji, na kwamba sekta hizo huwagusa Watanzania katika kawaida. 

Akizungumzia Wachimbaji Wadogo, Mahimbali amesema taarifa hizo za zitasaidia wachimbaji hao wachimbe sehemu zenye uhakika na kupelekea kupunguza hatari ya kupoteza fedha na mitaji yao kwa kufanya kazi bila kubahatisha.

Katika hatua nyingine, Mahimbali amesema kupitia Vision 2030, ushirikishwaji wa Watanzania utaimarika katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini na kwamba kufikia 2030

Kwa upande wa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii, Mahimbali amesema Serikali kupitia Wizara ya Madini inatatua kero za huduma za kijamii katika maeneo uchimbaji unapofanyika.

“Maeneo ambayo shughuli za uchimbaji zinafanyika tutaenda kutatua kero za wananchi wa pale kwa kuwajengea shule, vituo vya afya, barabara na miundombinu yote muhimu ili kuboresha mazingira yao, lakini sio wizara itaamua bali ni halmashauri zao kwa kuangalia vipaumbele walivyojiwekewea.” amesema Mahimbali. 

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Madini, Dkt. Abdul Rahman Mwanga amesema kuwa hakuna sehemu mashimo yatakapoachwa baada ya  shughuli za uchimbaji kukamilika kwa kuwa masharti ya leseni yanaitaka Kampuni zilizowekeza katika sekta ya madini kuwajibika katika kuacha mazingira salama kwa kuwasilisha mpango wa kufunga mgodi Serikalini na kupitishwa baada ya kuridhishwa na mpango huo.

Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri

Post a Comment

0 Comments