WAZIRI MAVUNDE ABAINISHA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA VISION 2030 KWA KAMATI YA BUNGE NISHATI NA MADINI

 



Na.Wizara ya Madini- Dodoma.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amebainisha mikakati ya namna utekelezaji wa Vision 2030 utakavyotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kufanya utafiti wa kina ili kubaini aina ya miamba na madini yaliyopo nchini.

Hayo yabainishwa leo Oktoba 3, 2023 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Utendaji kazi kuanzia mwezi Machi hadi Oktoba 2023.

Akitaja maeneo sita ya vipaumbele kwa ajili ya utafiti wa kina Mhe. Mavunde amebainisha kuwa utafiti katika  block I ni madini ya dhahabu , Almasi, bati na nikeli. Block II ni madini mkakati ya niobium, phosphate, dhahabu, nikeli, Shaba, bati, Helium na PGE.

Kwa upande wa Block III utafiti wa kina utafanyika katika madini ya Kinywe, Shaba , nikeli na dhahabu.

Akibainisha aina ya madini katika Block IV ,V na VI Mhe.Mavunde ametaja kuwa Uranium ,Helium, dhahabu, Chuma, lithium, Nikeli, Shaba, Tanzanite , kinywe.

Kwa upande wa madini mkakati ni pamoja na Vanadium,Titanium, chromium na uranium.

Akijibu swali la Mjumbe wa Kamati Tumaini Magesa Mbunge wa jimbo la Busanda mkoani Geita kuhusu mikakati ya wizara katika  utekelezaji wa Vision 2030, Mhe. Mavunde alisema kuwa tayari  wadau wa maendeleo katika sekta ya madini kutoka ndani na nje ya wameomba kushirikiana na wizara.

Mhe.Mavunde amefafanua kuwa mpaka sasa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM) imeomba kufanya utafiti kwa njia ya kurusha ndege  Kanda ya Kati katika mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga na Tabora.

Waziri Mavunde ameongeza kuwa taasisi ya Jiolojia ya nchini Israel (GSI) imeomba kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha utafiti wa kina kulingana na mpango mkakati utakaongoza kukamilisha Vision 2030 ifikapo mwaka 2030.

Akielezea hali ya utafiti ilivyosasa Mhe. Mavunde ameeleza kuwa utafiti wa kina wa High Resolution Geophysical Survey wa mwaka 2014 ulifanyika katika asilimia 16 na Low Resolution Geophysical Survey  wa mwaka 2004 na ulifanyika kwa asilimia 100 katika vipimo vya skeli kubwa ambavyo bado haikidhi upatikanaji wa taarifa za kina.

Mpaka sasa utafiti wa jiofizikia kwa High Resolution umefanyika kwa asilimia 16 , jiokemia 24 na jiolojia asilimia 97.

*VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI*

Post a Comment

0 Comments