TUMIENI MAGETI JANJA KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI

 

OR-TAMISEMI

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  imetoa rai kwa Serikali kuhakikisha wanaweka mageti janja kwenye vituo vya kukatia  tiketi ili kuongeza mapato na kuboresha huduma kwa watanzania

Rai hiyo imetolewa leo Mei 4, 2024 na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati  hiyo  Mhe. Justine Lazaro Nyamoga alipokuwa  akifanya majumuisho ya ziara ya kikazi kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na ujenzi wa soko la Kariakoo jijini Dar es salaam

Amesema haiwezekani kuona wananchi mpaka sasa bado wanapanga foleni kukata tiketi wakati mageti janja yameletwa na serikali ,lakini  hajafungwa jambo hili linawakera wananchi na9 kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Ameendelea kufafanua kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha inakusanya mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA  na kuwapunguzia adha wananchi ya kupanga foleni kusubiri huduma

Inshangaza kuona mpaka sasa wananchi wanapanga foleni kukata tiketi wakati katika kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ilikuwa inatakiwa wananchi kuwa na kadi maalum za huduma ya usafirishaji'amesisitiza  Mhe Nyamoga

Amesema si vizuri kuwaacha wananchi wanapanga foleni kukata tiketi  ambapo wanatumia muda mrefu ambapo kama serikali ni jukubu let kuhakikisha tunwarahisishia huduma wananchi

Aidha, wameipongeza serikali kwa kuhakikisha wanatumia wataalam wa ndani katika kuujenga mfumo wa matumizi ya mageti janja  ambao utasaidia kupunguza mianya ya rushwa na kuongeza mapato

Post a Comment

0 Comments