CHAMA CHA HISABATI TANZANIA YAJIVUNIA HARRIS WA FEZA BOYS

 

 

Mshindi wa Mshindano ya Mtihani wa Hisabati Afrika(EAMO) Mashariki na Kati 2023 Haris Israel Phares ambaye ni Mwanafunzi wa Feza boys akizungumza na waandishi habari katika halfa ya kukabidhiwa zawadi kutoka chama cha Hisabati Tanzania.


NA MWANDISHI WETU 

CHAMA cha Hisabati Tanzania (MAT/CHAHITA) kimetoa zawadi kwa mshiriki katika mashindano ya Hisabati Afrika mashariki na kati mwanafunzi  kutoka shule ya kimataifa ya Feza Boys Haris Israel Phares, Tukio hilo limefanyika leo Jumatatu tarehe 08,May 2023 chuo kikuu cha Dar es salaam kitovu cha hisabati Jijini Dar es Salaam.

Chama cha hisabati Tanzania ni taasisi iliyoanzishwa(MAT/CHAHITA) mnamo mwaka 1966 katika idara ya Hisabati chuo kikuu cha Dar es salaam, malengo ya kuanzishwa chama hiki ni kuendeleza ufanisi wa somo la hisabati.MAT/CHAHITA mojawapo ya kazi yake hapa Tanzania ni kuratibu mashindano ya mtihani wa hisabati kwa ngazi ya taifa na kitaifa ikiwa ni sehemu ya kutumiza malengo yake, kila mwaka chama kinaandaa mshindano ya mtihani wa hisabati kimataifa kwa makundi ya sekondari (O level na A level) yajulikanayo kwa jina la Junior and Senior contest hufanyika kila ifakapo mwenzi wa kumi(10)

MAT/CHAHITA inashirikiana na wadau wa Hisabati Afrika katika kuratibu mashindano ya mtihani wa hisabati Afrika ambayo inahusisha nchi za ukanda wa Afrika mashariki na kati (EAMO) ambao unashirikisha wanafunzi kutoka Tanzania, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Burundi na Sudan ya kusini. 


Mashindano EAMO mwaka yamefanyika 20,April 2023 nchini Rwanda na Tanzania ikatoa washiriki sita (6) ambao ni Hamza Mwangadu Mwammoto kutoka shule ya Feza boys, Derick evarist Kasumbai kutoka Feza boys, Haris Israel Phares kutaka Feza boys, Mwanamis Mashauri Halidi kutoka  Inspire Secondary school,Blessing  Edward Masanga kutoka Mbeya secondary na El-Gibbor Mtweva kutoka Mbeya secondary. Hatimaye Tanzania inawakilisha vizuri  na mwanafunzi ya shule ya Feza Haris Israeli Phares anayeshika nafasi ya kwanza kati ya washindi watatu walioshinda nafasi ya kwanza. 

Hivyo MAT/CHAHIT imempongeza kumpatia zawadi Haris Phares na kumtakia kila kheri katika mashindano ya mtihani wa hisabati kimataifa, Chama hiki kinaongozwa mkuu wa  idara ya Hisabati ambaye mkuu wa Idara Dkt. Sylvester Rugeihyamu amelezea kuwa mashindano yapo ya aina tatu (3) ambayo ni Afrika mashariki (EAMO), Afrika (PAMO) na Dunia (IMO). 

Malengo ya mashindano haya ni  kuongeza uelewa, ufaulu na utayari wa somo hisabati na pia Kuongeza motisha kwa wanafunzi kupenda somo la hisabati kuwapatia zawadi washindi, Kuleta ushindani kwa wanafunzi washiriki Hivyo leo tuanajivunia kuona mshindi(Watatu kati ya wanafunzi washindi wa kwanza) wa mashindano ya mtihani wa hisabati Afrika mashariki na kati (EAMO) anatokea Tanzania.


Viongozi wa chama cha Hisabati Tanzania pembeni kulia katibu katibu wa MAT/CHAHIT Dkt. Said A Sime katikati ni Mkuu wa Idara ya Hisabati Dkt. Sylvester Rugeihyama wakizungumza na waandishi wa Habari.


"Leo tunajivunia Tanzania kuwepo kwa kijana wetu Haris, ametuwakilisha vizuri katika mashindano ya mtihani wa Hisabati Afrika mashariki (EAMO) kwa kushika nafasi ya juu ya kwanza kwa washindi watatu wa nafasi ya kwanza" Aliongezea Dr. Sylvester Rugeimhyama.


Naye Mwanafunzi  Harris Phares amesema kuwa mtihani wa somo la hisabati ni rahisi sana tofauti na wanavyolichukulia.... Kwani yeye hufanya kwa muda mfupi sana kufanya mtihani wa hisabati. 

Naye Baba Mzazi wa Haris Mr. Israeli Phares Magesa amewashauri wazazi wazazi kuwasimamia watoto hasa wanafunzi katika misingi bora na pia aliwatoa shaka watanzania kuwa mwanae amejiandaa vya kutosha kwenda kuchukua tena medali katika mashindano ya mtihani wa hisabati Dunia na kuwashauri wanafunzi kutumia mitandao katika kujufunza na kuelemika. 

Mama Mzazi Haris Bi Aika Magesa amesititiza wazazi kuwa karibu na watoto wanafunzi kujua shida, changamoto na nna matatizo ya kiuchumi katika kufanikisha ndoto zao, alitolea mfano kwa mwanae humsaidia kumnunulia bando ya kuperuzi mtaandaoni njia inayomsaidia katika kujifunza, kuelemika na kufanya mashindano ya mitihani ya hisabati mtandaoni. 

Naye Mwalimu wa Shule ya Feza boys Mwl Hamza Salehe alimpongeza Haris kuwakilisha vizuri shule ya Feza boys na Tanzania kwa ujumla.


 Katika Mwalimu ya shule ya Feza Bw. Hamza Salehe akiwa pembeni yake kushoto Harris Phares na pembeni kulia ni Mama yake mzazi Haris Bi Aika Magesa. 



Post a Comment

0 Comments