DC SHAKA AWABANA WATU WAWILI WALIOUZA MLIMA KWA TSH MIL.20

 


📍Kilosa, Morogoro


🕹️ *WAUZA MLIMA T.SH 20 MILLIONI* 


📃 *DC Shaka awabana 2 Wengine  48 watafutwa na Jeshi la Polisi*


Na Mwandishi Wetu.


Jeshi la Polisi wilayani kilosa limewatia mbaroni watu wawili akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msowero A, Petro Sanga (Paroko) mwenzake, Awadh Ngajime kwa tuhuma za kuuza ardhi  (eneo la mlima) mali ya kijiji cha Msowero, wilayani Kilosa.


Pia, inaendelea kuwatafuta watu wengine 48 ambao wanaosadikiwa kuwa sehemu ya mtandao uliohusika kuuza kinyume na utaratibu ekari 1158 za Kijiji zilizopo katika mlima huo.


 Hayo yalibainika wakati wa mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wanachi katika Kata ya Msowero uliotishwa na Mkuu wa Wilaya ya KIlosa Shaka Hamdu Shaka mwishoni mwa wiki kijjijini hapo.


Shaka alisema kumekuwa na wimbi la uvamizi wa maeneo ya ardhi unaoonekana kukithiri siku hadi siku na baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa wakihusika kuyauza kinyume na sheria.


"Tuna kata saba ndani ya wilaya hii zinaongoza kwa migogoro ya ardhi ikiwemo hii ya Msowero mnaongoza mnavamia maeneo ya serikali, viongozi wapo mnashirikiana nao wengine kisha mnageuka mnasingizia viongozi wa wilaya mkoa na taifa kuwa wanakuja kupora ardhi yenu kumbe ni uongo kabisa.


*"Mmeuza mlima kinyume na utaratibu ekari 1,158 zote mmevamia na kuuza hii ni mali ya serikali ya kijiji kisha mnageuka kushutumu wengine kumbe wenyewe ndio wahusika, Ocd Huyu mwenyekiti wa kitongoji aliyeshiriki kuratibu mauziano na na kukiri mbele yangu kuwa  amelipwa T.  shs 500,000 na huyu aliuza eneo la mlima kwa sh 20,000,000 naondoka nao, pia naagiza watu wengine 48 waliohusika kwenye kuuza wajisalimishe vinginevyo watafutwe popote walipo na wafikishwa kwenye vyombo vya sheria," alisema*


Hata hivyo, Shaka alipiga marufuku na kuweka zuwio la kuendeleza shuhuli yoyote katika eneo la mlima unaodaiwa kuuzwa huku akisisitiza kuwa walioziwa maeneo hayo wametapeliwa na mlima huo bado ni mali ya Serikali.


"Viongozi mpo mnayaona kitongoji, kijiji, kata wote mnajua lakini mnalea uovu huu, haiwezekani kila aliyehusika kwenye hili hatabaki salama ili iwe fundisho kwa wengine, naomba wajuilisheni wote walionunua eneo lile wametapeliwa na hatutasita kuchukua hatua kwa yoyote atakaekaidi amri halali ya serikali.


Kibaya zaidi baada kufanya uovu mnatafuta watetezi ambao na wao kwa kukosa busara na vile  wanafuta umarufu wanalibeba jambo bila kulifanyia utafiti na kujiridhisha kumbe mnawaingiza mkenge.


Nilishangaa sana viongozi wa chama kimoja cha siasa wakilibeba jambo hili wakidai wananchi wananyanganywa ardhi wanapigwa na kuondoshwa katika maeneo yao, kumbe mumewalisha matango pori mnaficha uovu wenu na wao kwa kwa vile maarifa yao madogo wakaona ndio ajenda ya kuibeba, limebuma sasa warudi kukanusha uongo waliouaminisha umma wa watanzania. Alifafanua Shaka.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Msowero Abdalla Machera alimueleza mkuu wa wilaya kuwa katika siku za karibuni viongozi wa kisiasa wamekuwa wakifika katika maeneo yao huku wakilazimisha wananchi kupigwa picha na kutoa.



Post a Comment

0 Comments