NUKUU 3 ZA RAIS SAMIA KUHUSU UMUHIMU WA MATUMIZI YA MBEGU NA MICHE BORA KWA WAKULIMA

 


Na mwandishi wetu

Zikiwa zimesalia siku 5 kuelekea kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, tumekuletea nukuu 3 za Rais Samia alipozungumza katika majukwaa tofauti juu ya umuhimu wa Tanzania kujitosheleza katika uzalishaji wa Mbegu na Miche bora


1. "Serikali imeviboresha vituo  vya utafiti na mashamba ya uzalishaji mbegu kutokana na kujiingiza kwenye masuala ya uzalishaji mbegu za kisasa (high breed) na kwamba lengo ni nchi kuweza kujitegemea kwenye mahitaji ya mbegu" - Alizungumza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika Septemba 2023

Jijini Dar es Saalam


2. "Kilimo bila utafiti hatuwezi kwenda vizuri tumefika hapa tunapojisifia kwa sababu ya utafiti na uzalishaji wa mbegu.  Sasa tukiachia maeneo haya yachukuliwe tunakwenda kudumaza shughuli za utafiti na uzalishaji wa mbegu” -  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2023

jijini Mbeya.


3. “Tunataka ifikapo 2025 robo tatu ya mbegu zote zinazotumika hapa nchini zizalishwe hapa kama siyo kujitegemea kabisa. Tunataka mbegu zilizothibitishwa na zinazoendana na aina ya udongo wetu pamoja na kustahilimi mabadiliko ya hali ya hewa” - Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika Septemba 2023

Jijini Dar es saalam
Post a Comment

0 Comments