JESHI LA POLISI YAMNASA MUHUJUMU WA MIUNDO MBINU YA TANESCO

 




Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kusimamia mifumo ya ya kisheria ya haki jinai tarehe 21 Novemba, 2022  mtaa wa Mbozi Temeke lilimkamata Lusekelo Kalinga (47) Mkazi wa Sinza na hatimaye akafikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.


Baada ya mashauri yake kusikilizwa tarehe 2 Mei, 2024, mshtakiwa huyo alipatikana na hatia na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela  kuhusiana na kosa alilolitenda la kuhujumu miundombinu ya Shirika la umeme TANESCO.


Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na operesheni kali maalum ya kuzuia, kufuwatilia na kuwakamata  watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuvunja nyumba na kuiba televisheni na vifaa vya kielectroniki.  Operesheni hiyo ilianza mwezi Marchi, 2024 na inaendelea  imefanikisha  kumkamata Essau Fransis (27) @Makumba mkazi wa Makumbusho na wenzake (wanne) 4 na Televisheni thelathini na tano (35) zilizoibwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam zimepatikana huku Televisheni sita (6) tayari zimeshatambuliwa 


Jeshi la Polisi limewakamata, na linawahoji kwa kina watuhumiwa wanne ambao ni Javani Ochengi (36) Raia wa Kenya, mkazi wa Kimara, Yohana Mroso (20) mkazi wa Mbagala, Fransis Asangwile (34) mkazi wa Kongowe na Auston Mpanju (32) mkazi wa Tuangoma wanatuhumiwa kujipatia fedha kwa udanganyifu kwa kujinadi kuwa wao ni wakala wa mafunzo ya biashara, kutafutia vijana shule, vyuo, kazi au sehemu za utalii nje ya nchi.


Watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia kampuni ijulikanayo kwa jina la PROFFESION EXCHANGE PLATFORM (PEXPLA) kuwahadaa watu walipe  pesa ili wasaidie kupata nafasi wanazo hitaji kitendo kilichowezesha watuhumiwa hao wa ulaghai  kukusanya kiasi kikubwa cha pesa toka kwa wananchi kisha kutoweka.


Jeshi pia, limemkamata  na linamuhoji kwa kina Hassan Chambilia Sumilanda (28) @ Dr hassan mangena, mkazi  Sinza, kumekucha kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udangayifu kwa kudai  kuwasaidia watu kupata kazi au uhamisho jambo ambalo sio la kweli. 



Mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia fursa mbalimbali za hafla za kiserikali kupiga picha na viongozi wakubwa wa Serikali  na kuziweka katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kwa jiina la Hassani Mangena na kujitambulisha kuwa mtumishi wa Serikali kutoka Wizara ya afya kitengo cha mama na mtoto, wakati mwingine hujitambulisha kuwa  ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya afya Ustawi wa jamii na lishe na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. 


watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa  za kweli na linaahidi kuzitunza kwa siri na halitakuwa na huruma kwa mtuhumiwa yoyote anayejihusisha na vitendo vya kihalifu


Imetolewa na;

Muliro J. MULIRO - SACP

Kamanda wa Polisi

Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments