WAPINZANI WAMUECHE RAIS WETU DKT SAMIA SULUHU HASSAN AFANYE KAZI" CDE JOKATE

 🗓️04 April, 2024

📍Geita


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo MNEC amewataka Wapinzani kumuacha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan afanye kazi kwani mambo mengi waliuyokua wanayataka amewaruhusu bila kipingamizi cha aina yoyote.


"Wapinzani walikuja na Mambo mengi kwanza walitaka kumuona Rais na aliwakubalia, wakataka Mikutano ya hadhara akawaruhusu , na wakataka Maandamano Bado wameruhusuwa mwisho walisema Miradi haitakamilika lakini ninyi ni Mashahidi Miradi yote inaenda kwa Kasi na Mingine imekamilika mfano Bwawa la Mwalimu Nyerere alikuta ni asilimia 24 sasa limekamilika na limeshaanza kuzalisha Umeme"


"Wameona mwendo wa Rais Samia ni Mzuri, Hoja zao zote kazipangua, kazi anaipiga sasa wanaanza kuibua hoja zao zisizo na Maana za kibaguzi sasa sisi tunawaambia wamuache RAIS Samia Suluhu Hassan afanye kazi". alisema Komredi Jokate 


Aidha Komredi Jokate amewasihi Watanzania kuwakataa Viongozi ambao wanataka kuwagawa Watanzania kwa Dini, Ukabila na Ukanda lakini pia kuwakataa Viongozi ambao wanataka Kuvunja Umoja wetu. 


"Ndugu zangu leo hapa wote tukatae Viongozi wa aina yoyote wanaotaka kutugawa kwa Dini, Makabila au Ukanda watu hawa hawana nia njema na Taifa letu, mambo ya Ukabila na Ukanda Watanzania tukishayasahu tangu tulipopata Uhuru hivyo hatutaku kuyasikia wala kuyaona katika nchi yetu 


"Katika Kongamano la UVCCM tulilolifanya Zanzibar tulltoa maanzio yetu kuwa tutaulinda Muungano wetu kwa Namna yoyote Ile na hatutaruhusu mtu yoyote kuonyesha ishara ya kutugawa".


"Kama wanavurugana huko kwao ambapo moto unawaka, uwake huko huko wasitake kuruharubia Tanzania yetu" 


Aidha Awetaka Mabinti na kina Mama kuwakataa Viongozi ambao wanatumia Lugha za kumdogosha Mwanamke katika Uongozi amewasisitiza kuwa kama wao (Wapinzani) wameshindwa kuwawezesha Wanawake Kushika Nafasi za Uongozi ni wao huku kwetu (CCM)  Wanawake wanauwezo Mkubwa wa Uongozi ndio Maana tunaye Mwanamke Shupavu Dkt Samia Suluhu Hassan". Alisema Komredi Jokate.


#KulindaNaKujengaUjamaa

#SisiNaMamaMleziWaWana

#Kaziiendelee


Imetolewa na 

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa

Post a Comment

0 Comments